August 8, 2016

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI.

Dirisha la usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes na Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017 lilifungwa saa 6.00 usiku wa Jumamosi Agosti 6, 2016.

Hadi dirisha linafungwa, timu kadhaa hazikuwasilisha kabisa usajili wake licha ya kukumbushwa kwa njia mbalimbali na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Usajili wa msimu huu ni kama msimu uliopita kwamba unafanyika kwa njia au mfumo wa mtandao unaoitwa Transfer Matching System (TMS) ambao (server) yake au chombo chake cha kutunza kumbukumbu kipo Makao Makuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) - Uswisi.

Kwa kawaida mfumo huu upo chini ya FIFA na TFF hutoa taarifa kwa FIFA tarehe ya kufungua dirisha la usajili na kufunga.

Mfumo huu uhusisha pande tatu ambazo ni klabu, shirikisho (TFF) na FIFA. Kimsingi kazi ya usajili hufanywa na klabu ambako inajaza fomu kwa njia ya mtandao na hupakia viambatanisho kama vile mikataba ya wachezaji na picha za wachezaji.

Zoezi hili hufanywa na Meneja Usajili wa klabu husika wakati shirikisho hufanya kazi ya kuhakiki na kuidhinisha tu na FIFA huratibu na kuusimamia mfumo mzima. 

Kabla ya kutangaza kufunguliwa kwa dirisha la usajili hapo Juni 15, 2016 Shirikisho liliandaa kozi ya mafunzo ya usajili kwa klabu zote 64 zikiwa ni 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara; 24 zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza la StarTimes na timu 24 zitakazoshiriki Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017.

Baadhi ya timu hazikutuma wawakilishi, lakini ziko zilizofanya jitihada za kuomba usaidizi kwa kufika ofisini TFF kuomba usaidizi wa kufanya usajili na zilifanikiwa. Kwa Young Africans, licha ya kuwa hapa Dar es Salaam, haikuomba usaidizi wowote na hata walipokumbushwa kuhusu suala la usajili, hawakujibu kitu.

Young Africans ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili mfululizo msimu wa 2014/2015 na 2015/2016, ni moja ya vilabu ambavyo havikutuma mwakilishi kwenye kozi iliyofanyika Uwanja wa Taifa kwa siku tatu mfululizo ikigusa wawakilishi wa madaraja ya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

Meneja wa TMS wa Young Africans ni Katibu Mkuu hakuwahi kupata mafunzo ya TMS.

Hivyo sasa klabu zote ambazo hakuzituma usajili wake, hazina budi kuandaa utetezi utakaokwenda TFF ambao utatumwa FIFA yenye mamlaka ya kufungua dirisha, na utetezi huo ukikataliwa timu husika inabidi ishuke daraja ambalo halimo kwenye usajili wa mfumo wa TMS.


TFF kwa sasa inasuburi barua ya utetezi wa klabu ambazo hazikukamilisha zoezi la usajili ili iutume FIFA. Sambamba na hilo TFF inatathimini mwenendo mzima kisha itatoa taarifa kwa FIFA ili kuangalia namna gani ya kushughulikia maeneo yaliyokuwa na upungufu kwa sasa na baadaye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic