August 5, 2016


Mshambuliaji Frederic Blagnon amemalizana na klabu ya Simba na sasa ni mali ya klabu hiyo.

Blagnon aliyekuwa akikipiga katika kikosi cha Africa Sports cha Ivory Coast amesaini leo kuichezea Simba na kupewa jezi rasmi na Rais wa Simba, Evans Aveva.

Mshambuliaji huyo alikuwa kati ya wachezaji waliotikisa nyavu katika mechi za kirafiki ambazo Simba ilicheza mkoani Morogoro ilipokuwa imeweka kambi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV