August 12, 2016Pamoja na ujio wao wa kimyakimya, Waarabu wa MO Bejaia wamekumbana na ujanja wa aina yake jijini Dar es Salaam kwa kulipishwa bei kubwa ya kiwanja cha mazoezi tofauti na bei yake ya kawaida.

Waarabu hao wa Algeria walitua Dar usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii na kufikia katika Hoteli ya Bahari Beach, tayari kuikabili Yanga katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Licha ya kuwahi kote, wamepigwa cha juu na wamiliki wa Uwanja wa Boko Veterani wanaoutumia kujiandaa na mchezo huo ambapo wanalipa laki tano kila wanapokanyaga uwanjani hapo, kiasi ambacho ni tofauti na bei ya kawaida shilingi laki tatu.

Taarifa hizo zimepenyezwa na mtu wa karibu wa wamiliki wa uwanja huo ambaye alisema: “Hawa lazima walipe tofauti na timu nyingine, kawaida huwa ni laki tatu kila programu ya mazoezi, lakini utaanzaje mgeni ambaye tena anakuja kutafuta pointi kwa timu yako umpe kipaumbele? Haiwezekani na ndiyo maana tukawabana na sisi ili wakome.


“Walituambia kuwa wanaweza wakasalia hapahapa (Dar) wajiandae na mchezo unaofuata dhidi ya Mazembe, maana watakuwa ugenini kwa hiyo wanasema bora wakamalizie hukuhuku ishu zao, kule DR Congo waende kwa ajili ya mechi tu,” aliongeza.1 COMMENTS:

  1. unapoteza focus blaza sasa hiyo nayo habari? yaaan unaifanya kama blog ya udaku

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV