August 11, 2016



Kocha Hans van der Pluijm amesema kikosi chake hakijakata tamaa katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Pluijm raia wa Uholanzi, amesema bado wanapambana na watakachofanya ni kuibuka na ushindi dhidi ya Bejaia ambayo iliwafunga bao 1-0 kwao Algeria.

“Mechi itakuwa ngumu, lakini katika soka hauwezi kukata tamaa mapema tena kwa rahisi namna hiyo. Kama tutashinda, basi tuna nafasi bado,” alisema Pluijm.

Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake kabla ya kuiva Mo Bejaia ya Algeria katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa, Jumamosi.


Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja huo leo kabla ya mechi hiyo ya Jumamosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic