August 12, 2016


Wapinzani wa Yanga, Mo Bejaia wamefanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho inayotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho.

Mo Bejaia kutoka nchini Algeria walionekana wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo ambayo kama watashinda watakuwa wamesonga mbele hadi hatua ya nusu fainali kwa takribani asilimia 90.


Lakini Yanga pia wanataka kushinda mchezo huo kuinua matumaini yao ya kufikia hadi asilimia 60 za kuweza kusonga mbele.

Katika mechi ya kwanza ambazo zilikutana nchini Algeria, Bejaia walishinda kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV