August 16, 2016


Mshambuliaji hatari Alvaro Moratta aliyekuwa anakipiga Juventus ameeleza namna ambavyo amekuwa akihofia makali ya washambuliaji watatu wa Real Madrid, Karim Benzema, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo, maarufu kama BBC.

Lakini amesema kwa juhudi kubwa kabisa, Kocha Mkuu wa Madrid, Zinedine Zidane amempa hali ya kujiamini.

“Haikuwa rahisi, BBC ni kitu kingine kabisa. Umeona walivyofanikiwa. Lakini Zidane amenipa hali ya kujiamini na matumaini makubwa.


“Naipenda Madrid, lakini nilikuwa nina hofu kurejea hapa. Sasa nimerudi tena,” alisema Moratta ambaye alitolewa Juventus kwa mkopo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV