August 17, 2016

Mshambuliaji na nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ametupiwa dongo kuwa amenenepa na kasi yake imepungua tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016/17.


 
Aliyetamka maneno hayo ni beki wa kuliwa wa zamani wa Manchester United, Paul Parker ambaye amesisitiza kuwa Rooney, 30, alianza kuonekana kunenepa tangu katika mechi ya Ngao ya Jamii wiki mbili zilizopita.

Tangu kuanza kwa msimu huu kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho amekuwa akimpanga Rooney nyuma ya mshambuliaji wa kati Zlatan Ibrahimovic ambapo ameshafunga bao moja."Rooney ameongezeka uzito, huo ndiyo ukweli,” alisema Parker ambaye alicheza enzi za Sir Alex Ferguson kuanzia mwaka 1991 hadi 1996, kisha akaongeza:

“Anahitaji kubadilika na aonyeshe ubora wake, wakati watu wakiheshimu yote aliyoyafanya, huu ni muda wake wa kuendelea kuthibitisha ubora wake na kuachana na mambo ya historia, soka ni kuhusu kinachoendelea sasa.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV