August 17, 2016

Licha ya kuwa na ratiba ngumu ya mazoezi na michuano iliyo mbele yao tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016/17, bado Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho na mchezaji wake, Paul Pogba wamepata muda wa kufanya kazi zao nyingine nje ya timu.

   
Wawili hao ambao keshokutwa Ijumaa watakuwa kwenye Uwanja wa Old Trafford kuikaribisha Southampton katika mechi ya Premier League, walikuwa pamoja katika studio ndogo iliyopo ndani ya Hoteli ya Lowry kwa ajili ya kutengeneza tangazo la biashara.

Kocha huyo raia wa Ureno alionekana akiwasili katika hoteli hiyo akiwa na nguo kadhaa kwa ajili ya kazi hiyo.

Shabiki akiomba kusainiwa jezi yake nje ya hoteli hiyo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV