August 5, 2016


Baada ya mfanyabiashara, Mohammed Dewji kutangaza kutaka kununua hisa nyingi za klabu ya Simba, mashabiki wa timu hiyo sasa wanatembea kifua mbele na kuanza kuwatupia vijembe wale wote waliokuwa wakiwabeza kutokana na klabu hiyo kutokuwa na fedha nyingi hapo awali.

Hivi karibuni uongozi uliopo madarakani chini ya Rais Evans Aveva, ulikubaliana na wanachama wa klabu hiyo kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo ambapo katika mabadiliko hayo imetoa nguvu kwa Dewji kufanikisha azma yake ya kununua hisa nyingi klabuni hapo.

Kutokana na hilo, juzi Jumatano wakati Simba inajiandaa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Highlands mkoani Morogoro, mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakiwapokea wachezaji huku wakilitaja jina la beki wao wa zamani, Hassan Kessy ambaye amehamia Yanga.

Championi Ijumaa liliwasikia mashabiki hao wakisema Kessy amepishana na fedha za MO na atajuta kule alipoenda alipodhani ndiyo kutakuwa na fedha milele.

Mashabiki hao walienda mbali zaidi na kusema watamfanyia kitu mbaya wakikutana naye mtaani kwani kama inavyojulikana kwamba Kessy ni mzaliwa wa mkoani Morogoro na familia yake ipo mkoani humo (Gazeti la Championi haliungi hoja msimamo wao huo kwa kuwa michezo ni furaha na siyo vita).

Ikumbukwe baada ya Simba kukubali kufanya mabadiliko hayo, tayari Dewji ameshawakabidhi shilingi milioni 100 kwa ajili ya usajili wa wachezaji ambao watakuja kuunda kikosi bora cha Simba.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic