August 5, 2016


Uongozi timu ya Ruvu Shooting umetangaza jumla ya wachezaji tisa wapya iliowasajili kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu Bara huku ikimtema beki wake kisiki, George Michael Osei ‘Beki Katili’ kwa madai ya kushuka kiwango.

Beki huyo alipata umaarufu huo msimu wa 2014-2015 kufuatia kumkaba shingoni mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa Osei ni miongoni mwa wachezaji nane walioachwa na timu hiyo kutokana na madai ya kushuka kiwango chake.

“Sisi Ruvu tayari tumeshafunga usajili wetu kwa kusajili wachezaji wapya tisa ambao wameungana na wengine waliopo kambini mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

“Wachezaji hao ni Jabar Azizi (Mwadui), Richard Peter (Mbeya City), Elias  Emanuel (Polisi Moro), Clidel Liota (Mji Njombe), Chande Magoja na Fulzuru Maganga (JKT Mgambo), Shaibu Nayopa  (JKT Aljoro), Abdulrahiman Mussa (JKT Ruvu) na Renatus Kisasa akiwa kama mchezaji huru. 


“Lakini tumeacha wachezaji nane ambao tulikuwa nao hapo awali kufuatia benchi la ufundi kutoridhishwa na uwezo wao na mikataba yao kumalizika ambao ni Ally Khan, Yahaya Tumbo, Chagula Chagula, Juma Mpakala, Rashid Gumbo, Kulwa Mobi, Gidion Seppo na George  Michael Osei,” alisema Bwire.

1 COMMENTS:

  1. Kumwita "BEKI KATILI" hamumtendei haki kwani mpira si vita kama ilitokea hivyo ni mhemko tu kwa wakati huo lakini sio tabia yake katika maisha yake ya uwanjani au nje ya uwanja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic