Simba imetakiwa kuilipa Coastal Union kitita cha milioni tano, ikiwa ni sehemu ya fidia ya mchezaji Coastal Union kama fidia ya wachezaji; Abdi Banda, Ibrahim Shekwe na Hemed Hamis.
Uamuzi huo umefikiwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyokaa jana.
Lakini kitu kizuri zaidi, Simba imeonekana haina kinyongo kuhusiana na hilo na imesema italipa fedha hizo.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Raymond Wawa, amethibitisha kwamba Simba imekubali kulitekeleza hilo.
Shauri jingine lilikuwa ni Simba kumlipa fedha zake za malimbikizo ya mishahara aliyekuwa kocha wake msaidizi, Richard Amatre raia wa Uganda.
Simba pia imekubali kukutana na kumalizana na kocha huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment