August 30, 2016

TEGETE (KUSHOTO) AKIWA NA JABIR AZIZ, WOTE WANAKIPIGA MWADUI FC.

Klabu ya soka ya Yanga, imeonekana ina kesi ya kujibu kuhusiana na madai ya wachezaji Jerry Tegete, Omega Seme na Hamis Thabit.

Wachezaji hao wameonekana kuwa wana haki ya kulipwa fedha zao za usajili na klabu hiyo.

Makamu Mwenyekiti Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Raymond Wawa, amesema Yanga ina kesi ya kujibu.

Kwa mujibu wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa jana, Yanga imeonekana ina kesi ya kujibu lakini kesi zake zote zimesogezwa wiki ijayo.

Sputanza ndiyo ilifungua kesi hiyo ikiwawakilisha wachezaji hao akiwemo Tegete ambaye alikuwa mchezaji nyota na tegemeo la ufungaji kwa Yanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic