August 10, 2016


MKURUGENZI MTENDAJI WA MULTICHOICE TANZANIA, MAHARAGE CHANDE (WA PILI KULIA) AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWENYE OFISI ZA KAMPUNI HIYO JIJINI DAR ES SALAAM, LEO. WENGINE KUTOKA KUSHOTO NI MABOSI WA MULTICHOICE AMBAO NI SALUM SALUM, FURAHA SAMALU NA BARAKA SHERUKINDO.

Kampuni ya Multchoice Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa English Premier League ambayo inaanza rasmi Agosti 13.

Wakati wa uzinduzi huo kupitia DStv, Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania, Maharage Chande amesema mechi 300 kati ya 380 zitaonyeshwa Live.

Lakini kama utajumlisha mechi za Premier League ambazo ni Live pamoja na zile za Ligi Kuu Hispania, yaani La Liga, jumla zitakuwa ni mechi 760 ambazo zitaonekana kupitia DStv ndani ya SuperSport.


Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo, Maharage amesema pamoja na kuongeza mechi za Live, Watanzania hadi wenye king’amuzi cha Sh 23,500 nao wataona Live mechi za Premier League ambayo ni mechi maarufu zaidi ya soka duniani.

“Tunazidi kuwasogelea mashabiki wa soka na kuwapa chaguo kwa kila wanachotaka. Tumepunguza bei na kila king’amuzi sasa kitakuwa kinaonyesha live mechi za soka ingawa zinatofautiana wingi,” alisema.

DStv, ndiyo wakongwe zaidi katika biashara ya ving’amuzi na ndiyo king’amuzi kinachoonyesha mechi nyingi zaidi za soka.

Kwani pamoja na Premier League na La Liga, SuperSport ni magwiji katika uonyesha wa ligi nyingine mbalimbali kama FA Cup, Capital One (zote za England), pia Spanish Super Cup, Copa del Rey na German Cup.EVANS MHANDO WA TBC, ALISHINDA KING'AMUZI SAAAFI...

1 COMMENTS:

  1. wasitudanganye watwambie ukweli...kupunguza bei za visimbuzi si suluhu la wengi kuangalia mechi hizo. Wangepunguza bei za vifurushi vyao basi hapo ningewaelewa. Maana kifurushi cha 23500 huwezi kupata game za epl zote na kuna channel ya SELECT 2 ambayo kwa bahati huonesha mechi moja moja kwa mara moja

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV