August 11, 2016


MKURUGENZI MTENDAJI WA MULTICHOICE TANZANIA, MAHARAGE CHANDE (WA PILI KULIA) AKITANGAZA KUHUSIANA NA UAMUZI WA MATANGAZO YA LIGI KUU ENGLAND KWA KISWAHILI. WENGINE NI MAOFISA WA JUU WA KAMPUNI HIYO, KUTOKA KUSHOTO NI SALUM SALUM, FURAHA SAMALU NA BARAKA SHELUKINDO.

Wapenda soka wameonyesha kufurahishwa kutokana na uamuzi wa DStv kupitia SuperSport kuanza kutanga mechi za Ligi Kuu England kwa Kiswahili.

Uamuzi huo, unaonekana kuwafurahisha wengi na kusema itakuwa ni ahueni ya wao kuelewa mambo mengi wanayozungumza wachambuzi.

Katika maoni waliyotuma kwenye blog hii, wamesema kutumia lugha ya Kiswahili itasaidia watu wengi kufuatilia kwa ukaribu ligi hiyo.

Multichoice Tanzania, wamesisitiza kwamba wataendelea kutanua mengi kuhusiana na masuala ya uchambuzi katika lugha ya Kiswahili inayohusiana na ligi hiyo.

SuperSport itarusha Live hadi mechi 300, hii ni kati ya mechi 380 za ligi hiyo maarufu katika soka duniani na kufanya utamu kwa mashabiki kuongezeka zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic