September 17, 2016

Vijana wa Arsena Wenger, Arsenal wametoa dozi tamu kwa Hull City katika Premier League kwa kuwafunga mabao 4-1 katika mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa  KCOM, leo Jumamosi.

Katika mchezo huo, Hull City ambayo pia ilipata majanga kwa mchezaji wake, Jake Livermore kupewa kadi nyekudu katika dakika ya 40, pia staa wa Arsenal, Alexis Sanchez alikosa penalti katika dakika ya 41.


Mabao ya Arsenal latika mchezo huo yaliweka wavuni na Alexis Sanchez dakika ya 17na 83, Theo Walcott dakika ya 55 na Granit Xhaka dakika ya 90 ambaye alifunga bao zuri la shuti kutoka mbele kidogo ya eneo la katikati ya uwanja.

Matokeo mengine ya Premier League
Leicester City 3 – 0 Burnley
Manchester City 4 – 0 AFC Bournemouth
West Bromwich Albion 4 – 2 West Ham United

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV