September 17, 2016

Presha ya mchezo wa Mwadui FC dhidi ya Yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga ilikaribia kuvuka mipaka kwa makocha wa timu hizo ambao walitaka kushikana wakati wa mapumziko.
Julio alipokuwa akifafanua jambo siku za nyuma katika mkutano na waandishi wa habari.

Picha kamili ilikuwa hivi, mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao ulimalizika kwa Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0, ulikuwa na presha kuwa wakati wa mchezo na hata kabla ya kuanza kwa kipute hicho, huku kukiwa na tambo nyingi kutoka kila pande.

Wakati wa mchezo huo, makocha wote walionekana kuwa bize kuelekeza huku mara kadhaa wakilalamika, wakati wa mapumziko Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm ghafla alioenekana akibishana na Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambapo haikujulikana ubishi wao ni kuhusu nini.
Julio na Pluijm wameshakutana mara kadhaa, hii ilikuwa msimu uliopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Wakati wawili hao wakibishana, ilionekana Pluijm akipandisha 'mzuka' na na kufoka kwa sauti ya juu hata alipokuwa akitenganishwa na Julio na wasaidizi wake, kuona hivyo, Julio naye akaongeza sauti lakini hawakuweza kushikana, wakaondoka kuelekea vyumbani.

Julio aliondoka huku akizungumza na msaidizi wa Pluijm, Mwambusi.

Baada ya mchezo huo, Julio alipoulizwa juu ya suala hilo alisema yeye alikuwa akilalamikia baadhi ya maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo ambayo aliona hayakuwa sahihi, ndipo Pluijm akaingilia na kuanza kumjibu kwa ukali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic