Baada ya Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa kudai kuwa kuna program zake ambazo hazifanyiwi kazi kila anapoziwasilisha kwa mwajiri wake, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), majibu yametolewa na mwajiri wake huyo.
Mkwasa alitoa malalamiko yake hayo siku kadhaa zilizopita ambapo ni baada ya Taifa Stars kukamilisha ratiba ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kufungwa na Nigeria bao 1-0 nchini Nigeria, ambapo alidai kuwa kuna program ameziwasilisha na hazijafanyiwa kazi na shirikisho hilo.
Alisema kuwa kutofanyiwa kazi kwa program zake hizo kunachangia kuzorotesha kazi yake na kuomba apewe ushirikiano ili kurahisisha majukumu yake hayo.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alipoulizwa juu ya suala hilo alisema: “TFF ni taasisi kubwa, kila sehemu ina kitengo chache kinachohusika na majukumu yake, hivyo suala la Mkwasa anaweza kuwasilisha katika kitengo husika ili asaidiwe.”
Mkwasa alitoa malalamiko yake hayo siku kadhaa zilizopita ambapo ni baada ya Taifa Stars kukamilisha ratiba ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kufungwa na Nigeria bao 1-0 nchini Nigeria, ambapo alidai kuwa kuna program ameziwasilisha na hazijafanyiwa kazi na shirikisho hilo.
Mkwasa |
Alfred Lucas |
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alipoulizwa juu ya suala hilo alisema: “TFF ni taasisi kubwa, kila sehemu ina kitengo chache kinachohusika na majukumu yake, hivyo suala la Mkwasa anaweza kuwasilisha katika kitengo husika ili asaidiwe.”
0 COMMENTS:
Post a Comment