September 13, 2016

Kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes, jana usiku aliendelea kuwa na wakati mgumu baada ya kushuhudia timu yake ya sasa ya Sunderland ikipata kichapo cha mabao 3-0 na kuendelea kuwa kwenye hali tete katika msimamo wa Premier League.
 
Moyes ambaye alipata kipigo hicho kutoka kwa timu yake ya zamani pia, Everton ambayo aliifundisha kwa miaka 11, mabao yote yaushindi yakiwekwa wavuni na Romelu Lukaku aliyetupia hat-trick.

 
Msimamo wa Premier League ulivyo sasa.

Defoe wa Sunderland akiwa hoi baada ya kukosa bao.

David Moyes


Kwa matokeo hayo Moyes anaendelea kuiongoza Sunderland bila ushindi wowote tangu kuanza kwa msimu huu ambapo sasa inashika nafasi ya 19 kati ya timu 20 katika mechi nne ikiwa na pointi moja.

Lukaku alifunga mabao hayo katika dakika ya 60, 68 na 71. Kabla ya mabao hayo ilikuwa imemchukua Lukaku dakika 1,139 kufunga bao katika ligi hiyo lakini ndani ya dakika 11 tu akafunga mabao matatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV