September 13, 2016

Mchezaji staa wa Barcelona, Lionel Messi akishirikiana na wenzake wawili Neymar na Luis Suarez ambao walikuwa wakijulikana kwa kifupi kama MSN wamefanya kazi nzuri kwa kuipa kichapo Celtic mabao 7-0 kwenye Uwanja wa Camp Nou katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao matatu katika mechi moja ‘hat-tricks’ mara nyingi zaidi kuliko wote katika michuano hiyo ya Ulaya.
Wafungaji wa Barcelona ni Messi aliyefunga katika dakika 3, 27 na 60, Neymar (50), Andrés Iniesta (59) na Luis Suarez (75 na 88).

Kutokana na mabao hayo, Messi sasa amefikisha hat tricks sita akimzidi Cristiano Ronaldo wa Real Madrid mwenye hat tricks tano.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV