September 17, 2016

Baada ya kufanya uzembe wikiendi iliyopita na kupoteza pointi tatu, Barcelona imeamka na kutoa kipigo cha nguvu katika Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’, leo Jumamosi.

Barcelona imeichapa Leganes mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Butarque.

Mabao ya wababeo hao yamefungwa na Messi aliyefunga mawili katika dakika ya 15 na 55, Luis Suarez dakika ya 31, Neymar dakika ya 44 na Rafinha dakika ya 64.

Katika mchezo huo, Messi, Suarez na Neymar amabo ushirikiano wao unaitwa MSN walionyesha makali ambapo uashirikiano wao ulikuwa ni wa juu na walikuwa wakipeana pasi wao kwa wao katika kufunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV