September 17, 2016

Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein maarufu kwa jina la Tshabalala au Zimbwe Jr ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Simba kwa mwezi Agosti, 2016.

Zimbwe Jr ambaye katika siku za hivi karibuni na hata katika msimu uliopita amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Simba, alikabidhiwa tuzo hiyo leo Jumamosi kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Uhuru ambao timu yake ilishinda bao 1-0.


Zimbwe alikabidhiwa tuzo yake hiyo uwanjani hapo na Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geophrey Nyange 'Kaburu' pamoja na Mkurugenzi wa EAG Group, Imani Kajula.

Makabidhiano ya tuzo hiyo yalienda sambamba na zawadi ya fedha shilingi 500,000.

Licha ya kuwa na namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza cha Simba, Zimbwe pia amekuwa akipata nafasi katika kikosi cha TaifA Stars.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV