September 7, 2016


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema tayari wameshakamilisha mfumo wa utumiaji wa tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, na muda wowote zitaanza kutumika.

Ni kwa muda mrefu serikali ilitangaza kuweka mfumo wa tiketi hizo kwenye viwanja inavyovimiliki vya Uhuru na Taifa, lakini suala hilo lilionekana kama kusuasua kabla ya hivi karibuni kutiliwa mkazo na hatimaye kukamilika.

Awali ilielezwa kuwa, Jumapili iliyopita ndiyo serikali itakabidhiwa mfumo huo baada ya kukamilika, lakini zoezi hilo likaahirishwa kutokana na shughuli za kiserikali kuingiliana.

 Nape alisema: “Kila kitu kimekamilika na nimehakikishiwa hilo na wale tuliowapa kazi hiyo, ile ratiba ya awali ya kukabidhiana nimeiahirisha mimi na si mwingine kwa sababu siku tuliyopanga awali mimi nilikuwa Dodoma kwenye shughuli nyingine za kiserikali.”

Nape alisisitiza kuwa, wikiendi hii ndiyo wanatarajia kulifanya zoezi hilo la makabidhiano.


SOURCE: CHAMPIONI.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV