September 16, 2016

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib amezua hofu kwenye kikosi hicho kama ataweza kucheza mechi ya kesho dhidi ya Azam FC mara baada ya kuumia mguu wa kushoto jana Alhamisi katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veteran, Boko jijini Dar.

  Ajib alikutana na mkasa huo mara baada ya kugongana na beki wa timu hiyo, Novaty Lufunga wakati walipokuwa wakigombania mpira.


Championi Ijumaa, lililokuwepo uwanjani hapo lilishuhudia tukio zima lilivyokuwa ambapo ilianzia kwa wachezaji hao kutaka kuonyeshana umwamba ambapo Ajib alikuwa anataka kumtoka Lufunga ambaye hakukubali na kujikuta akimchezea faulo iliyopelekea mshambuliaji huyo kutoendelea na mazoezi.

Mara baada ya kuumia Ajibu alitolewa huku akiwa amefungwa bandeji jambo ambalo lilizua hofu kwa mashabiki wa timu hiyo wakati kikosi hicho kikiwa na siku moja tu kabla ya kuwavaa Azam.

Baada ya mazoezi hayo, Ajib aliliambia gazeti hili: “Daaah! Nimeumia hii sehemu inauma sana.” baada ya hapo hakutaka kuzungumza zaidi.

Alipoulizwa Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema: “Siwezi kusema kuwa atakosa mchezo wa Azam au la, ni mpaka nimfanyie uchunguzi zaidi.”
 


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV