September 12, 2016

Simba pamoja na jana kuichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 2-0 lakini bado akili yao ipo kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga huku ikitenga michezo miwili ya ligi hiyo ambayo ina jumla ya dakika 180 ikiwa ni kipimo chao cha mwisho juu ya hatma yao kabla ya kuvaana na Wanajangwani hao. 

Kabla ya mchezo wa jana, Simba ilikuwa tayari imecheza mechi tatu, ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mechi mbili na kusuluhu moja. Hata hivyo, timu hizo sasa kila moja imebakiza mechi mbili mkononi kabla ya kukutana Oktoba Mosi, mwaka huu.


Benchi la Ufundi la Simba kwa kauli moja limeeleza kuwa litatumia matokeo ya michezo yake hiyo inayofuata kwa kuanzia na wa Azam FC kisha Majimaji kama kipimo cha hatma yao watakapokutana na Yanga.


Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ameeleza kuwa uhalisia watakaouona katika mechi hizo mbili utakuwa ni kipimo tosha kupata taswira ya matokeo ya mechi yao dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.


Logo za Yanga na Simba

Mashabiki wa Yanga na Simba

Mchezo baina ya Yanga na Simba huwa unakuwa na presha kubwa kuanzia kwa mashabiki hasi wachezaji.

Simba inacheza na Azam, Septemba 17 kabla ya kuvaana na Majimaji, Septemba 24.

“Tumebakisha michezo michache kabla ya kucheza na Yanga, tunajua ni mechi ngumu na yenye hisia kubwa kwa mashabiki. Kiuhalisia tunahitaji matokeo mazuri lakini kitaalamu tutatumia matokeo ya mechi mbili za mwisho zinazokuja kupata taswira ya itakavyokuwa tutakapocheza na Yanga.


“Tutaanza na Azam ambao nao kila msimu wanafukuzia ubingwa, kwa maana hiyo haitakuwa mechi nyepesi kwetu. Nyingine itakuwa ni dhidi ya Majimaji ambao nao ni wazuri pia, kwa hiyo utaona hizi zinaweza kuwa mechi zetu za kipimo tosha kabla ya kukutana na Yanga.


“Tukiibuka na ushindi katika mechi hizi zote mpaka na ya Yanga angalau sasa tunaweza kuwa na hatua moja katika mafanikio ya msimu huu, tunahitaji zaidi ushindi katika mechi hizi,” alisema Mayanja.


Kwa upande wa Yanga ambayo imebakiza michezo miwili dhidi ya Mwadui FC na Stand United kabla ya kucheza na mahasimu wao, yenyewe imecheza michezo mitatu mpaka sasa pia ikiwa na matokeo ya kushinda mechi mbili na kusuluhu moja.


Alipotafutwa Kocha wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm kuzungumzia mchezo huo, alisema kwa kifupi: “Hapana, kabla ya Simba nina michezo miwili kwanza ya ku-dili nayo, nikimaliza hiyo ndiyo naweza kuiangalia mechi ya Simba sasa.”

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic