September 12, 2016

Beki wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Boniface Pawasa, ameangalia mfumo unaotumiwa na Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, kisha akasema kama kweli anataka wafunge mabao mengi, basi ni lazima aubadilishe.
Omog

Pawasa

Pawasa amekosoa mfumo huo wa Omog wa kuwapanga pamoja washambuliaji Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib kwa wakati mmoja huku akisema washambuliaji hao wanacheza soka la kufanana.


“Ukiangalia uchezaji wa Mavugo ni kama namba kumi, pia Ajib anacheza kama hivyo, yaani wote wakiwa katika kikosi cha kwanza utaona anakosekana mshambuliaji wa mwisho ambaye muda wote anatakiwa kuwa kwenye eneo la hatari la wapinzani.


“Kwa mfumo anaoutumia Omog, hana budi kuwachezesha Ajib na yule Muivory Coast (Frederic Blagnon) au Mavugo na huyo jamaa (Blagnon) kwani yeye nimemuona ndiye anaweza kucheza kama mshambuliaji wa mwisho tofauti na hao wengine.


“Kama Omog akiendelea kuwatumia zaidi Ajib na Mavugo kwa pamoja, basi watakuwa na kazi kubwa ya kufanya kwenye kusaka ushindi, wanaweza kushinda lakini si kirahisi,” alisema Pawasa.



 


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic