September 18, 2016




Kikosi cha Kilimanjaro Queens kimetinga katika fainali ya Kombe la kwanza la Chalenji kwa wanawake baada ya kuwatwanga wenyeji wa michuano ya hiyo Uganda kwa mabao 4-1.

Uganda ambayo kikosi chao cha wanaume wakiwemo wachezaji kama Emmanuel Okwi kimefuzu kucheza Afcon, dada zao walionekana kuushindwa kabisa mziki wa Kilimanjaro Queens.

Ushindi huo sasa unaikutanisha Kilimanjaro Queens katika mechi ya fainali dhidi ya Kenya ambao wamefanikiwa kutinga baada ya kuwang’oa Ethiopia kwa kuwachapa mabao 3-2.

Katika mechi hiyo ya Kilimanjaro Queens mjini Jinja, wenyeji walionekana wamezidiwa kwa kiasi kikubwa na Queens walipata bao la mapema katika dakika ya 6 kupitia Donosia Daniel.

Kama vile wenyeji wangeweza kuamsha matumaini lakini walitandikwa bao la pili mfungaji akiwa Mwanahmisi Omari katika dakika ya 17 na Stumai Abdallah akapigilia msumari wa tatu dakika ya 31.

Kilimanjaro Queens walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao 3-0 na Asha Rashid ‘Mwalala’ alipigilia msumari wa mwisho huku wenyeji wakipata bao moja la ‘kuchafua gazeti’.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic