September 14, 2016

Baada ya kupata kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City katika Manchester Derby, habari nyingine ambayo siyo nzuri kwa wadau wa timu hiyo ni hii hapa.Beki na kiungo wa Manchester United, Philip Anthony Jones maarufu kwa jina la Phil Jones anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na matatizo ya goti aliyoyapata akiwa mazoezini.
Kocha wa timu hiyo Jose Mourinho amethibitisha juu ya tatizo hilo na kusema kuwa uchunguzi unaendelea.

Jones amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara kiasi cha kushindwa kuwa na uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza, ambapo karika dirisha la usajili lililopita alihusishwa kuuzwa au kutolewa kwa mkopo kutokana na kutopata nafasi mara kwa mara.

Jones amekuwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kati, pembeni na mara kadhaa kama kiungo mkabaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV