September 18, 2016

Wiki za majanga kwa Manchester United zimeendelea baada ya kupoteza mchezo wa tatu mfululizo ndani ya wiki mbili, hiyo ni baada ya kukubali kufungwa na Watford mabao 3-1, leo Jumapili.

United ilipoteza mchezo wa Manchester Derby dhidi ya Manchester United katika Premier League, ikapoteza dhidi ya Feyenoord katika Europa League na sasa ni dhidi ya Watford katika Premier League.

Kipigo hicho kimeweka rekodi kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Watford kupata ushindi dhidi ya wababe hao kutoka Jiji la Manchester, huku Kocha wa United, Jose Mourinho akiwa haamini alichokiona kwenye mchezo huo.

Mabao ya Watford katika mchezo huo yalifungwa na Etienne Capoue, Juan Zuniga na Troy Deeney wakati lile la vijana wa Jose Mourinho likiwekwa wavuni na Marcus Rashford.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV