September 18, 2016

 
Mara baada ya Klabu ya Lyon ya Ufaransa kutangaza kuwa dili la kumsajili mshambuliaji Emmanuel Adebayor limekufa kutokana na sababu kadhaa ikiwemo kuwa na hofu ya kumkosa mchezaji huyo mwakani kwa mwezi mmoja au miwili kutokana na kuwa atatkiwa kwenda kushiriki katika michuano ya Afrika, mchezaji huyo amejibu mashambulizi kwa ukali.

Adebayor ambaye siyo mtu wa kupenda kuweka mambo kwa uficho amefunguka mambo mengi yaliyotokea likiwemo hilo suala la yeye kwenda kuichezea timu yake ya taifa ya Togo, akiita sababu zilizotolewa ni za kipuuzi.

Adebayor ambaye ana umri wa miaka 32 alitarajiwa kusajiliwa na timu hiyo ya Yfaransa inayoshiriki katika Ligue 1 amefafanua hivi:"Wamesema hivyo? (kuhusu michuano ya Afrika), huo ni upuuzi walinifuata baada ya kufuzu michuano ya Afrika, walijua lazima nitacheza, wameanza kutafuta sababu zisizo za msingi, watajiua wao wenyewe.

“Mimi ni nahodha wa nchi yangu, kwa nini nisende kuliwakilisha taifa langu, vipi kama nahodha wa Ufaransa asiende kuichezea nchi yake kwenye Euro?

"Walizungumza na kocha wangu wa Togo na hawakuomba huduma maalum kuhusu mimi. Nilijua kuwa hakuna dili kati yetu Jumamosi (jana)…

 
“Nilipofika pale (Lyon) nilizungumza na kocha na niijua naenda kupimwa afya na kusaini mkataba lakini ajabu nilipoanza kuzungumza na kocha wao, akaanza kuniuliza maswali yasiyo ya msingi, ananiuliza kama nimeona, kama nina watoto, kama alitaka kujua taarifa zote hizo si angeangalia kwenye mtandao….

"Nimecheza soka kwa kiwango cha juu kwa miaka 15 na nimefanya kazi na makocha wenye uwezo wa juu duniani kama [Arsene] Wenger, [Jose] Mourinho, [Didier] Deschamps, [Roberto] Mancini.

"Aliniuliza kwa nini sikuendelea kuichezea  Crystal Palace. Nilimweleza mimi huwa nacheza katika timu zinazowania ubingwa, kilichotokea kwenye timu hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuichezea timu inayopigana kutoshuka daraja na ndiyo maana baadaye niliona hiyo timu haiendani na mimi.

"Mimi nipo imara, nilitakiwa kuwa nimekufa tangu mwaka 2010, hivyo sina hofu ya kitu chochote, nitaendelea kufanya kitu kingine, kilichotokea ulikuwa ni ukurasa wa kuchekesha," alisema Adebayor.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV