September 9, 2016

Ama kweli Masau Bwire hakosi la kusema hata kama akifungwa! Safari hii ameibuka na jipya baada ya awali kumbeza straika wa Simba, Laudit Mavugo ambaye alisema mashabiki watamuita straika huyo kinyozi kwani hataweza kufanya lolote dhidi yao. 


Kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, Bwire ambaye ni Ofisa Habari wa Ruvu, alitamba vijana wake watamdhibiti Mavugo kiasi kwamba atakosa la kufanya, lakini haikuwa hivyo kwani ndiye aliyefunga bao la pili kwa Simba kwenye ushindi wa mabao 2-1.

Baada ya mchezo huo, Bwire aliliambia Championi Ijumaa kuwa: “Unajua Watanzania wengi wanampaisha sana Mavugo wakati ni mchezaji wa kawaida tena sana.

“Kiwango chake si cha kutisha na hata mabao yake anayoyafunga ni ya kawaida, kama leo (juzi) bao lake ni la bahati, mabeki wetu walijichanganya kidogo wakamuacha peke yake ndiyo akafunga.

“Ninao vijana wa darasa la nne nawafundisha soka, kila siku nawaona wanafunga mabao kama yale ya Mavugo kwani ni rahisi mno na sidhani kama kuna mtu anaweza kukosa akiwa eneo lile.”

Tayari Mavugo ameshafunga mabao mawili msimu huu baada ya kucheza michezo mitatu akiwa na Simba. Bao lake la kwanza kufunga ilikuwa kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Ndanda wakati Simba iliposhinda mabao 3-1.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV