September 19, 2016

Baada ya kipigo cha tatu mfululizo, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameonyesha kuwa na hasira na kutofurahishwa na aina ya ukabaji wa beki wake wa kushoto, Luke Shaw katika mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Watford.

Man United ilifungwa mabao 3-1 na wapinzani wao hao katika Premier League.

Mourinho akizungumza na Shaw baada ya kutolewa katika mchezo wa jana.
Mourinho amenukuliwa akisema: "Bao la kwanza tulilofungwa na Man City na lile la pili la Watford unaweza kuna kuna uhusiano, bao la Man City (Aleksandar) Kolarov alikuwa na mpira na mchezaji wangu badala ya kwenda kumkata alimpa nafasi ya kufanya maamuzi.”

Katika kosa hilo, Mouringho alikuwa akimzungumzia kiungo wake, Henrikh Mkhitaryan.


Shaw alipokuwa kabla ya bao.

Shaw akielekea kwa mpinzani.
 
Shaw akishuhudia bao la pili likiingia.


Jose Mourinho

Henrikh Mkhitaryan katika mechi ya Man City.

Mourinho akaendelea kusema: "Hili la pili nalo, (Nordin) Amrabat alikuwa na mpira kisha beki wetu wa kushoto alikuwa umbali wa mita 25 kutoka alipo mpinzani badala ya kuw amita tano. Lakini hata unapokuwa katika kita 25 unatakiwa kumfuata na kumdhibiti, lakini yeye alisimama akimsubiri.

"Hili ni kosa la kiufundi lakini linahitajia uelewe wa kisaikolojia.

"Naweza kugawa vipigo hivyo katika sehemu tatu, kwanza ni makosa ya waamuzi, ambayo yapo nje ya uwezo wangu.

"Lakini katika mechi ya Man City unajua kilichotokea katika dakika ya 55 (kipa wa City Claudio Bravo alipomkwatua Wayne Rooney). Kilichotokea pia katika mechi ya Feyenoord walipofunga bao wakati kuna mtu alikuwa ameotea.

"Pili, kumekuwa na kukosa bahati na hiyo ni sehemu ya mchezo.

"Tatu ni suala lililopo mkononi mwangu, kuboresha kikosi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic