September 17, 2016

Mchezo umemalizika hapa kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, wageni Yanga wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC, yote yamefungwa na Donald Ngoma.
  
Dakika ya 90 + 4: Mwamuzi anamaliza mchezo.
 
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaongeza dakika 4 za nyongeza.
 
Dakika ya 90: Donald Ngoma anaifungia Yanga bao la pili, Msuva alipiga pasi kwa Niyonzima ambaye naye alipiga krosi iliyotua kichwani kwa Ngoma, akatupia wavuni.
 
Ngoma GOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!


Dakika ya 89: Mchezo unaendelea, wachezaji wote wamenyanyuka.
 
Dakika 87: Wachezaji wa Yanga, Dante na Twite, wanagongana hewani wakati wakiwania mpira. Mchezo umesimama wanatibiwa.
 
Dakika ya 82: Yanga wanapata kona, inapigwa akini inaokolewa.
 
Dakika ya 80: Msuva anabaki yeye na kipa, anapiga shuti lakini linadakwa na kipa wa Mwadui.
 
Dakika ya 75: Ngoma anazuiliwa na mabeki watatu wa Mwadui baada ya kuumiliki mpira.
 
Dakika ya 72: Yanga bado inaongoza 1-0, mashabiki wa Mwadui wanaonekana kuwa wapole.
 
Dakika 67: Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Mahadhi, anatoka Deusi Kaseke.
 
Dakika ya 61: Faulo hiyo inapigwa lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 60: Mwadui wanapata faulo nje kidogo ya eneo la 18 la Yanga.

Dakika ya 52: Mwadui wanapata kona, inapigwa lakini mpira unatoka nje.
  
Dakika ya 50: Mchezo unaendelea ukiwa na presha kubwa.
 
Kipindi cha pili kimeanza. 
 
Baada ya kutengenishwa, Julio na Pluijm wakaingia vyumbani huku kila mtu akiwa anamlalamikia mwenzake.
 
Mara baada ya mwamuzi kukamilisha kipindi cha kwanza, wakati timu zikielekea kwenye vyumba, makocha wa timu hizo Julio wa Mwadui na Pluijm wa Yanga wakaanza kurushiana maneno, ikabidi watu wengine wa mabenchi yao ya ufundi kuingilia kati kuwatengenisha.
 
KIPINDI CHA KWANZA KIMEKAMILIKA
Dakika 45: Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza.

Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kamusoko ambaye aliumia ugoko, ameingia Haruna Niyonzima.
 
Dakika ya 42: Yanga bado inaongoza bao 1-0. Timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 40: Mchezo unaendelea, Kamusoko anaendelea lakini Niyonzima anaendelea kupasha misuli pembeni ya benchi la timu yake.
 
Dakika ya 8: Mchezo umesimama kwa muda Kamusoko wa Yanga kaumia. Haruna Niyonzima anapasha misuli nje ya uwanja.
 
Dakika ya 30: Mchezo ni mgumu kwa kuwa Mwadui nao wanajibu mashambulizi na wanakuwa wanapanda kushambulia. Mabeki wa Mwadui wanapambana kwelikweli na washambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe.
 
Dakika ya 28: Mchezo umesimama kwa muda, Mwadui wapo makini na wanajibu mashambulizi ya Yanga.
 
Dakika ya 25: Msuva anakosa nafasi baada ya mpira wake wa kichea aliopiga kupaa juu ya lango akiwa karibu kabisa na lango.


Dakika ya 22: Yanga wanakosa bao baada ya Tambwe kupiga shuti linalotoka nje ya lango.
  
Yanga wanapata bao la kwanza kupitia kwa Amiss Tambwe baada ya mabeki wa Mwadui kufanya uzembe. Deus Kaseke alipiga mpira wa faulo mabeki wa Mwadui na kipa wao wakazubaa katika kuokoa, Tambwe akatupia wavuni.
 
Dakika ya 5: Tambwe GOOOOO!!!!!!!!

Dakika ya 1: Yanga wanaanza kwa kasi

Mchezo umeanza.

chMchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Mwadui Vs Yanga kwenye Uwanja wa Kambarage.

1. Ali Mustafa
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Andrew Vicent
5.Kelvin Yondani
6. Mbuyu Twite
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Deusi Kaseke

Subs;
- Deogratius Munishi
- Oscar Joshua
- Juma Mahadhi
- Yusufu Mhilu
- Obrey Chirwa
- Haruna Niyonzima
-Canavaro.           


 Kikosi cha Mwadui FC
1.Lucheke Mussa 18
2.Masoud Chollo 14
3.Yasin Mustapha 23
4.Joram Mgeveko
5.Idd Mobi 4
6.Zahoro Jarah 6
7.Hassan Kabunda 17
8.Moris Karike 22
9.Rashidi Ismail 19
10.Paul Nonga 13
11.Miraji Athuman                        


Waamuzi wa leo
1.Ahmad Simba-Kagera
2.Robert Luhemeja-Mwanza
3.Geofrey Msakila-Geita
Official Rebeca Mlokozi-shy.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic