September 17, 2016


Mjadala wa mchezaji gani ni bora kati ya Lionel Messi na Crtistiano Ronaldo umeendelea, ambapo safari hii nguli wa mchezo wa soka, Pele wa Brazil ameaingilia kati na kumtaja yupi ambaye anaamini kwake ni bora zaidi.

Awali kiungo wa zamani wa Barcelona, Xavi aliibuka na kusema Ronaldo ni mchezaji mzuri lakini Messi ni bora zaidi na kuwa Ronaldo ana bahati mbaya kucheza soka katika kizazi ambacho Messi anacheza, Ronaldo alikuja juu na kumjibu mchezaji huyo kwa dharau kuwa hana muda wa kujibishana naye na yeye (Ronaldo) ni bora ndiyo maana kapata tuzo tatu za Fifa Ballon d'Or.

Straika wa zamani wa Barcelona, Samuel Eto’o naye alijitokeza na kusema kuwa Messi ni bora zaidi ya Ronaldo.


  Pele naye amesema kuwa katika miaka 15 iliyopita, Messi amekuwa ndiye mchezaji bora kuliko wote.

"Ningeweza kutaja majina ya wengine lakini kati ya miaka 10 hadi 15 nafikiri Messi amekuwa mchezaji mwenye kiwango cha juu.

"Tulikuwa na wachezaji wengi bora. Cristiano Ronaldo naye ni mzuri lakini Messi anaweza kutengeneza na kufunga.

"Cristiano Ronaldo ni kama Ronaldo wa Brazil, ni mzuri katika kufunga, hilo halina ubishi lakini ukitakiwa kumtaja mchezaji bora ni Messi," alisema Pele.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV