September 4, 2016


Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameendelea kujifua kwa kasi ikiwa ni maandalizi ya kurejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu sasa.

Ronaldo aliumia wakati wa michuano ya Euro na yeye kulazimika kutolewa wakati wa mechi ya fainali, lakini Ureno ikafanikiwa kubeba ubingwa.


Ronaldo amekuwa akiendelea na mazoezi makali kwenye Viwanja vya Valdebebas jijini Madrid, ili kuhakikisha akirejea kikosi, basi anakuwa kiwembe kwelikweli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV