September 4, 2016Timu ya taifa ya Uganda, The Cranes imefuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuichapa Comoro kwa bao 1-0.

Ushindi huo umeifanya Uganda kufikisha pointi 13 sawa na vinara wa kundi D, Burkina Faso na kuwaacha Comoro na Botswana wakirejea nyumbani kama ilivyo kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Bao la Uganda limefungwa na Farouk Miya mbele ya mashabiki kibao wa Uganda jijini Kampala leo. Michuano hiyo itafanyika mwakani nchini Gabon.

Uganda inafuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika ambalo ilishiriki mara ya mwisho mwaka 1978 ikiwa chini ya Kocha Mserbia, Sredejovic Milutin 'Micho' aliyewahi kuinoa Yanga.


Kufuzu kwa Uganda, huenda kutakuwa changamoto kwa Tanzania kwamba kuna mambo yanayotakiwa kupunguzwa kama ubinafsi na zaidi kuangalia maendeleo kwa ajili ya taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV