September 19, 2016

Mara baada ya  timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kuipa kichapo Congo Brazzaville katika hatua ya tatu kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana itakayofanyika mwakani, wachezaji mastaa wa Tanzania wametoa maoni yao.

Wachezaji hao ni Mbwana Samatta wa Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ambao waliwahi kucheza pamoja kwenye timu ya TP Mazembe.

Samatta (kulia) akiwa katika majukumu yake ya Genk.

Samatta akiwa mazoezini Genk.
 Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wote wawili wamezungumza kwa ufupi kuwapongeza vijana hao.

 

Samatta akiwa mazoezini Genk.

Thomas Ulimwengu ‏ndiye aliyeanza kwa kuandika: “Mnaliwakilisha taifa lenu vyema sana. Well done boys.”
 Baadaye Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars, aliandika: “Unaweza kuwa msingi imara wa mafanikio tuanzie hapa.”

Mchezo huo wa kwanza wa hatua hiyo ulifanyika kwenye Uwanja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2 ambapo mshindi wa hapo atasonga mbele kwa kufuzu moja kwa moja katika michuano hiyo ya vijana.

Serengeti Boys wakishangilia bao.

Ulimwengu akiwa TP Mazembe

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic