September 9, 2016

Klabu ya Simba imeripotiwa kumalizana na Oman Club ya nchini Oman ikidaiwa kumpeleka mshambuliaji wake, Danny Lyanga kwa makubaliano ya kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mmoja.

  


Championi Ijumaa limepenyezewa taarifa hiyo kutoka kwa mtu wa ndani wa Wekundu hao akieleza kuwa mshambuliaji huyo ameondoka tangu juzi na ukiachana na makubaliano ya mkopo pia kuna maelewano ndani ya mkataba huo kwamba kama Oman watamuelewa zaidi wanaweza kumsajili moja kwa moja.

“Lyanga ameondoka tangu jana (juzi) na yupo kule kwa makubaliano ya mkopo, huo ndiyo ukweli uliopo lakini ndani ya mkataba pia kuna kipengele juu ya maelewano ya kumnunua moja kwa moja kama wataridhika naye na kila kitu kimekuwa ‘fixed’ katika ishu hiyo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Lakini hata hivyo, ulipotafutwa uongozi wa Simba kulitolea ufafanuzi suala hilo, ulikiri kuwa Lyanga yupo Oman lakini kwa makubaliano ya kufanya majaribio kwa wiki mbili na si kwamba tayari wameingia kandarasi na timu hiyo juu ya mchezaji huyo.


Lyanga

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alieleza: “Ni kweli Lyanga ameondoka jana (juzi), amekwenda Oman Club, lakini ni kwa ajili ya majaribio ya wiki mbili, bado hatujaingia mkataba wa mkopo na klabu hiyo.

“Tunategemea kwamba atakapomaliza wiki mbili hizo na baada ya kupewa majibu ndiyo tunaweza kujadili juu ya hatma yake kulingana na walivyomuona huko Oman. Kimsingi kwa Lyanga tumepata mwaliko wa klabu hiyo tu kwa sasa.”

Taarifa ambazo zilipatikana ni kuwa tayari mchezaji huyo alishaanza kazi tangu jana, ambapo aliwasili mazoezini na kujumuika na wenzake.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic