September 9, 2016

Straika mkongwe wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amefunguka mengi katika mahojiano marefu ya kwanza aliyoyafanya na kituo cha runinga na MUTV huku akigusia mchezo wa Manchester Derby dhidi ya Manchester City.


Guardiola sasa ni kocha wa Man City


Zlatan amesema kuwa anaamini yeye na kocha wake, Jose Mourinho wanaelewana falsafa kwa kuwa ni watu wa ushindi lakini alipoulizwa kuhusu Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alisema: “Nilikuwa namjua Guardiola wa Barcelona lakini huyu wa sasa simjui.”
 
Katika mahojiano hayo ambayo yamerushwa hewani leo Ijumaa, Zlatana amesema kuwa Guardiola ni kocha mzuri na alichokuwa akikijua kipindi cha nyuma kuhusu kocha huyo hawezi kusema ndivyo alivyo sasa.

“Kwa sasa simjui, kipindi kile kila mtu alijua ni kocha mzuri na nsiyo maana alifanikiwa, anafanyaje kazi leo, mimi sijui, anaendeleaje hilo nalo sijui kwa kuwa siyo kocha wangu,” alisema Zlatan.


Guardiola alipokuwa akifanya kazi pamoja na Zlatan ndani ya Barcelona.

Kuhusu Mourinho alisema: “Nampenda na ninamuelewa kwa kuwa ni mtu ambaye anakwambia ukweli bila kuwa na konakona, kama haupo vizuri anakwambia, hata mimi napenda mtu wa aina hiyo.

“Anao uwezo wa kuipa timu mafanikio ndani ya muda mfupi.”

Straika huyo mwenye umri wa miaka 34 alisema: "Kwangu mimi mechi kubwa ndiyo ambazo ninazitaka, nimecheza katika derby nyingi, El Clasico, Inter/Milan derby, Ajax na Feyenoord na hata PSG/Marseille.

"Moja ambayo nilikuwa nimeikosa ni hii, nipo tayari," alisema mchezaji huyo raia wa Sweden.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV