September 12, 2016

Tiketi za kuingilia uwanjani hivi sasa zitakuwa ni kama kadi za benki.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa matumizi ya tiketi za kielektroniki zenye mfumo wa kadi kama za benki, hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.Waziri Nape wakati wa uzinduzi wa tiketi za elektroniki.

Waziri Nape wakati wa uzinduzi wa tiketi za elektroniki.

Katika uzinduzi huo, Nape alisisitiza mfumo huo ambao uliwahi kutumika lakini ukasitishwa kutokana na changamoto lukuki, alisema ujio wake ni mwisho wa wizi wa mapato pamoja na kujua idadi kamili ya watu walioingia uwanjani pamoja na taarifa kamili ya kila mtu atakayeingia uwanjani.

Kwa kufungua tu, tayari Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamepatiwa kadi zao zitakazowawezesha kuingia uwanjani.

Nape alisema kadi hizo mbali na malipo ya kuingilia uwanjani, pia zinaweza kufanya malipo mengineyo. Mzabuni wa mfumo huo ni Kampuni ya Selcom.


  “Kumekuwa na malalamiko mengi kuwa tiketi zinaibiwa katika mgawanyo wa mapato, lakini mfumo huu ndio dawa pekee ya kumaliza tatizo hili na hakutakuwa na wizi tena.

Uwanja wa Taifa (kulia) unavyoonekana kwa juu, pembeni ni Uwanja wa Uhuru.
“Maana kila sehemu itapata mgawanyo wake kihalali. Kila ukilipia tiketi, gawio la wizara litakwenda moja kwa moja, TRA watakata zao na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) watapa gawio lao moja kwa moja, tofauti na mfumo wa awali,” alisema Nape ambaye alisema mfumo huu mpya utawezesha kunasa taarifa zote za kila mtu atakayeingia uwanjani, ikiwa ni faida ya usalama na idadi kamili ya watazamaji.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV