MAMA wa Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu, Bi. Miriam Sepetu ameingia kwenye headlines mitandaoni baada ya kutofautiana na mkali wa nyimbo za singeli, Man Fongo.
Kwa mujibu wa Man Fongo akihojiwa na
baadhi ya vyombo vya habari amekiri kutokea kwa mfarakano huo huku
akisisitiza kuwa hajatenda kosa lolote kwa mama Wema.
“Hii ilianza wakati akiwa safarini
na wasanii wenzake wakitoka Kahama kwenda wilayani Mureba kufanya shoo
ya fiesta. Wakiwa kwenye gari,”
“Christian Bella akanza kwa kusema kuwa kila anapoposti kitu chochote mtandaoni anatukanwa.”
Ndipo Man Fongo akauliza, “Unatukanwa na nani na kisa ni nini?”
Maelezo yaliendelea kutolewa na Bella huku wasanii wengine wakichangia hiyo maada na baadaye maada ikawa imeisha.
Kwa mujibu wa Man Fongo anadai baadaye
alitumiwa ujumbe wa matusi kwenye simu yake na mama Wema huku
akishutumiwa kuzungumza maneno machafu yenye nia ya kuichafua familia ya
Sepetu.
Msikie Man Fongo: “Wamemtumia
meseji mama yake na Wema kwamba ninaisema familia yake wakati mimi
Manfongo muhuni na muhuni siku zote hatuna muda wa kumzungumzia mtu,
riziki yangu naisaka tangu nipo kitaani sina muda wa kujibishana na watu
sasa Mama Wema ananitumia meseji za matusi”
Msikie Mama Wema: “Kwanza
kama utakuwa umesoma SMS yangu niliyomtumia nilimwambia kwamba Amani
nakuheshimu sana hasa baba yako ambae mpaka sasa namuheshimu ila matusi
ambayo umeanza kunitukana huko ulipo nimeyapata sasa endelea…..”
“Sasa mimi ndio wakumshtaki maana
amenisema vibaya huko walipokuwa na watu wake ziarani nimeumia sana mimi
kama mzazi, Manfongo bado mtoto mdogo sana kwangu na mimi”..
Bonyeza play kuitazama hii video Mama Wema Sepetu akieleza tofauti yake na Man Fongo
0 COMMENTS:
Post a Comment