September 9, 2016

Staa wa zamani wa Barcelona, Xavi amesema kuwa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ni mchezaji mzuri laini anachokosea ni kujifananisha au kuzaliwa katika utawala wa Lionel Messi wa Barcelona.
   

Upinzani baina ya Ronaldo na Messi umekuwa mkubwa na umedumu kw amiaka kadhaa katika soka la Ulaya kwa kuanzia kwenye La Liga huku wawili hao wakiwa wametwaa tuzo nane za Ballon d’Or katika miaka nane iliyopita.
Mashabiki wa Ronaldo na Messi


Ronaldo na Xavi katika mechi ya Barcelona na Real Madrid

Ronaldo na Xavi wakatihuo Ronaldo alipokuwa Manchester United.
“Ronaldo ni mchezaji mzuri kwa nafasi yake, tatizo ni kuwa kuna mwingine ambaye ni bora kwenye historia ya soka na anaendelea kucheza.

“Ronaldo ni kifaa lakini kumfananisha na Messi, kwangu mimi na kwa mtu anayejua soka ni vitu vitiwili tofauti.

“Messi ataendelea kuwa namba moja kwa muda wote mpaka atakapoona inatosha, ni mchezaji bora labda uwe shabiki wa Real Madrid ndiyo unaweza kukataa,” alisema Xavi ambaye kwa sasa anaichezea Al Sadd SC ya Doha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic