October 9, 2016


Baada ‘ya kuanza vizuri, Kocha wa muda wa England, Gareth Southgate amesema ana imani ataendelea kufanua vizuri zaidi.

Southgate amesema kikosi cha ‘Three Lions’ kina uwezo wa kufanya vizuri zaidi.

"Tukiwa pamoja, tutafanya vema. Tukisaidiana tutaweza kufika lakini kila mmoja atimize jukumu lake kwa asilimia za juu," alisema.

Lakini amesisitiza anahitaji ushirikiano kutoka kila upande ili kufanya anachotaka au wanachotaka Waingereza wote.

Southgate amechukua nafasi ya Sam Alladayce ambaye alikumbwa na kasha ya rushwa.


Katika mechi yake ya kwanza, ameiongoza England kuitwanga Marta kwa mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV