October 9, 2016


Kinda Farid Mussa amerejea mazoezi kwenye kikosi cha Azam FC baada ya kukosekana kwa muda kadhaa.

Ilielezwa kwamba Farid Mussa alikwenda mjini Morogoro kutokana na masuala ya kifamilia hii ikiwa ni baada ya kufanya mazoezi muda mrefu akisubiri kwenda Hispania.

Mambo yanaonekana kuwa magumu kwake kwenda kujiunga na Tenerife ambayo tayari imemsajili lakini inasubiri kibali.

Mabingwa wa Afrika Mashariki, Azam FC wameendelea na mazoezi yao ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuwavaa Stand United, Farid akiwa mmoja mmoja wa wachezaji walioshiriki mazoezi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV