October 9, 2016


Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe ameweka wazi alivyofurahishwa na Kocha Joseph Omog.

Hans Poppe amesema Omog raia wa Cameroon ni kati ya makocha wachache wasiotaka utani katika suala la nidhamu.

Hans Poppe amesema, Omog amekibadilisha kikosi hicho kwa kuongeza nidhamu zaidi.


“Unajua hata wale watukutu msimu uliopita, sasa wamekaa sawa na wanafanya kazi yao.

“Ni kocha anayelipa kipaumbele suala la nidhamu,” alisema.

Hans Poppe alisema nidhamu ndiyo muongozo sahihi katika maisha ya binadamu, hivyo anaamini Omog pamoja na mambo mengi akilishikilia hilo, atafanikiwa.


Kwa sasa Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 17 kileleni baada ya kucheza mechi saba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV