Mara tu baada ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, kuikacha timu hiyo na kuondoka, winga wa timu hiyo, Simon Msuva, ametoa kauli kuwa kuondoka kwa Pluijm ni pigo kwao ingawa hawana jinsi ya kufanya kwani kocha huyo amefanya maamuzi hayo kwa mapendekezo yake.
Pluijm aliandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake wa kocha mkuu wa timu hiyo mara baada ya viongozi kudaiwa kumleta nchini kocha Mzambia, George Lwandamina kubeba mikoba yake. Yanga kwa sasa ipo mikononi mwa Juma Mwambusi aliyekaimu nafasi ya kocha mkuu.
“Najua siku zote nimekuwa nacheza kwa uwezo wangu ila kwa kiasi kikubwa Pluijm alikuwa anatusaidia vitu kibao, kuondoka kwake naweza kusema inaniuma na sijafurahia sana kuona ametuacha muda huu, japo kwa upande wangu sijajua sana ni nini ambacho kimesababisha hadi akafikia hatua ya kufanya maamuzi hayo,” alisema Msuva.
0 COMMENTS:
Post a Comment