October 28, 2016


PLUIJM
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, ameondoka katika nafasi yake hiyo huku akiacha historia ya jina la tawi jipya la Kocha Pluijm Branch litakalokuwepo Ilala Machinga Complex jijini Dar es Salaam.

Kumbumbuka kocha huyo ni mwanachama wa klabu ya Yanga, alichukua kadi yake kabla ya kuiacha Yanga na kwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia, halafu baada ya Marcio Maximo mambo kumshinda, akarejea.

Tawi hilo lilipangwa kutambulishwa juzi Jumatano mara baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakati Yanga ilipocheza na JKT Ruvu lakini haikuwezekana.

Mwenyekiti msaidizi wa tawi hilo, Said Manzi, amesema tawi hilo wamelipa jina hilo kutokana na kutambua mchango na mafanikio yake aliyoipa Yanga katika kipindi chote alichokuwepo.

Manzi alisema, tawi hilo limepangwa kuzinduliwa rasmi wikiendi hii kabla kocha huyo hajaondoka kurudi kwao baada ya kusitisha mkataba wake ambapo hadi sasa wana wanachama 20 waliojiandikisha na kupatiwa kadi zao za Benki ya Posta.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic