October 9, 2016

MWENYEKITI WA YANGA, YUSUF MANJI
Uongozi wa klabu ya Yanga, umeitisha mkutano wa dharura ulipangwa kufanyika Jumapili.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumapili ya Oktoba 23 na ukumbi utatangazwa.

“Ukumbi utatangazwa, lakini uongozi unapenda kutangaza kuitishwa kwa mkutano huo,” alisema.

Hakuna kilichoelezwa kuhusiana na ajenda za mkutano huo lakini kuna uwezekano mkubwa ukawa ni kuhusiana na suala la kukodisha.

Hivi karibuni, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limetoa taarifa ya kutaka kufuatwa kwa taratibu likionyesha kupinga mkataba wa ukodishwaji wa Yanga.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya BMT iliyosainiwa na Katibu wake, Mohamed Kiganja inaonekana kujichanganya kiasi kikubwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV