Kampuni ya uuzaji matairi nchini ya Bin Slum Tyres Ltd,imeendeleza utamaduni wake wa kulidhamini tamasha la ‘Kandanda Day’,ambalo litafanyika Oktoba 15,mwaka huu katika uwanja wa Jakaya M Kikwete Park,Kidogo Chekundu.
Mratibu wa tamasha hilo,Fatma Dahir,amesema kwamba wanaishukuru kampuni hiyo inayoongoza kwa uuzaji matairi nchini kwa msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya tamasha hilo linalobebwa na kauli mbiu Dawati na Mpira.
“Kwanza kabisa tunapenda kuchukua fursa hii,kuishukuru sana kampuni ya Bin Slum,kwa kutuamini na kuwa pamoja zaidi ya miaka miwili katika kuhakikisha tamasha hili linaendelea kuboreka mwaka hadi mwaka,”alisema na kuongeza
“Kwa mwaka huu,kauli yetu mbiu ni Dawati na Mpira, ambayo lengo lake kuu ni kuhakikisha sisi kama wanamichezo tunaunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha shule zetu zina madawati ya kutosha,hivyo tunaamini kwa ushirikiano wa wanamichezo wanaounda kundi la Kandanda kwenye ukurasa wa facebook na wadau wengine,tunaweza kuchangia kitu kwa ajili ya elimu yetu.”
Fatma alisema, kwamba wanaamini udhamini wa fedha walioupata kutoka Bin Slum,utakua chachu ya ulifanikisha tamasha la mwaka huu,kuwa bora zaidi na kuweka historia kwa wanamichezo watakaoshiriki na shule itakayopata msaada wa madawati.
Kwa upande wa mwakilishi wa kampuni ya Binslum Tyres Ltd, Bwana Salim Said Al Jabry, alisema kwamba wameamua kuendeleza utamaduni wao wa kuchangia tamasha la kandanda pamoja na kuuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati nchini.
“Binslum Tyres tunafuraha kubwa ya kuendelea kuwa sehemu ya udhamini,ikumbukwe huu ni mwaka wa tatu kwa kampuni yetu kudhamini tamasha hili,ambalo kwetu ni faraja kuona wadau wanakutana pamoja na kushiriki pia kuisaidia jamii kupitia mchezo wa kandanda,”alisema Al Jabry na kuongeza:
“Kwa hiyo mwaka huu mbali na kutoa jezi kwa timu mbili mwenyeji ya Team Dizo Moja na Team Ismail,lakini pia tumetoa kiasi cha fedha kipatacho milioni moja kwa ajili ya kuchangia mchango wetu wa madawati na shughuri zingine za uendeshaji.”
Mwaka huu tamasha hilo linatarajia kushirikisha timu mbalimbali za makampuni ambazo zitacheza katika mfumo wa ligi,kabla ya mshindi kupatikana katika mchezo wa fainali.
Mratibu wa Kandanda Day
Fatma Dahir
0 COMMENTS:
Post a Comment