October 13, 2016


Klabu ya Chelsea imepiga bongo la bingo baada ya kuingia mkataba mpya na Nike.

Nike ni kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ambayo imekubali kumwaga pauni milioni 900 kwa miaka 15.

Mkataba huo unakuwa mnono zaidi hats kushinda ule wa Manchester United wanaolamba pauni million 700.

Nike na Adidas ni wapinzani wakubwa kwa kampuni zinazotengeneza vifaa via michezo. Adidas ndiye ilikuwa na mkataba mkubwa zaidi ya Manchester United.

Sasa Nike imeingia na kuonyesha inaweza kwa kumwaga fedha zaidi Chelsea.


Pamoja na kutofanya vizuri sana, Chelsea inabaki kuwa moja ya timu zinazouza sana jezi na mmliki wake, Roman Abramovich amepanga kuiimarisha kwa kumwaga mamilioni ya usajili wakati wa dirisha dogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic