Katika kunogesha tamasha la Kandanda Day,wachezaji wanaounda kikosi cha Dar City FC,wanatarajia kushuka katika dimba la uwanja wa Jakaya M Kikwete Park,Kidogo Chekundu,Jumamosi wiki hii.
Kiongozi wa timu hiyo, Athuman Tippo ‘Zizzou’, alisema kwamba wameamua kushiriki tamasha la mwaka huu ili kuunga mkono,kampeni inayoendelea nchini ya ukusanyaji fedha kwa ajili ya madawati katika shule mbalimbali nchini.
“Sisi kama wadau wa soka,tumeamua kushiriki katika tamasha la kandanda day,ili kutoa mchango wetu kwa jamii kupitia michezo,tunaamini wachezaji wanaoshiriki tamasha hilo wa Dar City,wanakila sababu ya kuwa sehemu ya mchango huo,”alisema Tippo na kuongeza:
“Kwa maana hiyo,kikosi changu ambacho kitashuka dimbani kitakuwa kimekamilika na kitakuwa kimesheheni wachezaji wengi waliowahi kutamba na wanaoendelea kutamba katika soka la nchi hii.”
Baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi hicho ambao walipata kuzitumikia klabu za soka za Simba na Yanga ni Juma Kaseja,Salvatory Edward,Elimboto Nkumbi,Haruna Moshi’Boban’,George Masatu,Kassa Mussa,Shaaban Kado na Shaaban Ramadhan.
Tamasha hilo,linatarajia kushirikisha timu mbalimbali za makampuni na taasisi lina na kampuni ya matairi nchini Bin Slum Tyres Ltd,kampuni ya simu ya mikononi Smart,Michuzi Blog,Galacha na Coca Cola.
Imetolewa na Mratibu
Mohamed Mkangara
0 COMMENTS:
Post a Comment